Posts

KAMPUNI YA KAHAMA OIL MILL'KOM' YAJENGA JENGO LA KISASA HOSPITALI YA KAHAMA

Image
Jengo la kisasa la kukaa wananchi wanaofika kusubiri kuona wagonjwa ndugu na jamaa wanaolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama ambalo limejengwa kwa msaada wa makampuni ya muwekezaji mzawa ya Kahama Oil Mill kwa gharama ya Sh milioni 11.8 pamoja na kuweka mabenchi ya kukaa watu. Na Patrick Mabula - Kahama Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Anamringi Macha ameipongeza Kampuni ya Kahama Oil Mill (KOM) inayomilikiwa na mwekezaji mzawa kwa hatua ya kujenga jengo la kisasa la kupumzikia wananchi wanaofika katika hospitali ya wilaya hiyo kuwajulia hali wagonjwa. DC Macha ametoa pongezi hizo jana Jumatatu mjini Kahama wakati akifungua jengo hilo na kueleza kuwa uwepo wa jengo hilo ni msaada kwani utawaondolea adha wananachi kukaa juani na wakati wa masika kunyeshewa na mvua wanapofika kuona wagonjwa ndugu na jamaa zao waliolazwa hospitalini hapo. Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Lucas David alisema hospitali hiyo ilikuwa inakabiriwa n...

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAJANE DUNIANI : WAJANE WAKUMBUSHWA KUACHA KUKURUPUKA KUOLEWA

Image
Na Sumai Salum - Kishapu Wanawake wajane wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wametakiwa kujipa moyo na kupata muda wa kutosha wa kupumzisha akili kabla hawajaamua kuingia kwenye mahusiano mengine mapya kwa lengo la kuondokana na changamoto na migogoro ya mahusiano baada ya kuwa wameondokewa na wenza wao. Hayo yamesemwa leo Juni 23,2020 na  Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Kishapu Bw. Joseph Swalala ikiwa ni siku ya maadhimisho ya Wajane Duniani yenye kauli mbiu isemayo “HAKI NA ULINZI KWA WAJANE MSINGI IMARA KWA MAENDELEO YA JAMII”  ambapo ameiasa jamii kutoendeleza mila na desturi kandamizi na zilizopitwa na wakati zenye lengo la kuwanyima wanawake wajane haki zao za umiliki mirathi pindi wanapofiwa na waume zao. “Sheria ya mirathi inaeleza baada ya mme kufariki dunia mke anatakiwa awe msimamizi ila mila na desturi kandamizi zimekuwa zikipindisha sheria hii kwa kuchagua ndugu mme wa marehemu kuwa ndie msimamizi na mali zikishaisha anamterekeza , lakin...